Thursday 5 April 2007

Ujinga + Uroho = Uharibifu

Ujinga ni adui wa maendeleo Mwl. JK Nyerere alisema, Ujinga sio ule wa kutokwenda shule tu bali pia ule wa mwenye kwenda shule halafu asitumie elimu yake katika kufanya mambo yake. Kwa mfano Kumpa Daktari mkuu Uwaziri wa Mawasiliano, na yule aliyesomea mawasiliano ukwambia asimamie Afya. Kumpa Uwaziri wa sanaa mtu aliyesomea Uinjinia. Uroho ni ule wa mtu aliyepewa nafasi ya kuhudumia jamii akatumia nafasi hiyo kujinufaisha yeye binafsi bila kujali. na ukisha jumlisha hayo mawili unapata jawabu la UHARIBIFU, nao ni kama vile kufanya manunuzi yasiyo muhimu kwa nchi, kuuza rasilimali za nchi bila kujali kelele za wananchi, kuvunja kila palipojengwa, kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi na kuchukua pesa za nchi na kuzihamishia ugenini......

Karibuni kwenye Mlinganyo wa Bongo

Najua karibia wabongo wote mlio nje na ndani ya bongo mnayo nia ya kujikomboa kutoka kwenye umasikini wa kujitakia tulionao na tunaondelea kuwa nao. Wengi wenu mmekwenda shule ya kutosha ya kuweza kufanya mabadiliko na kuondoa uozo uliopo katika nchi iliyo jaaliwa utajiri wa kila aina. Kikwazo ni wachache walioko madarakani wenye uchu wakutumikia matumbo yao zaidi kuliko Uchungu wa nchi yao. sasa huuu ni mlinganyo wa kwa kuweka hadharani mabovu yao ili waone aibu, tuwaaibishe wayaone wanayofanya..... leta picha yako yenye kuonyesha ubovu uliopo na utoe jawabu la ubovu huoo kama unaweza .....weka hapa