Thursday 5 April 2007

Ujinga + Uroho = Uharibifu

Ujinga ni adui wa maendeleo Mwl. JK Nyerere alisema, Ujinga sio ule wa kutokwenda shule tu bali pia ule wa mwenye kwenda shule halafu asitumie elimu yake katika kufanya mambo yake. Kwa mfano Kumpa Daktari mkuu Uwaziri wa Mawasiliano, na yule aliyesomea mawasiliano ukwambia asimamie Afya. Kumpa Uwaziri wa sanaa mtu aliyesomea Uinjinia. Uroho ni ule wa mtu aliyepewa nafasi ya kuhudumia jamii akatumia nafasi hiyo kujinufaisha yeye binafsi bila kujali. na ukisha jumlisha hayo mawili unapata jawabu la UHARIBIFU, nao ni kama vile kufanya manunuzi yasiyo muhimu kwa nchi, kuuza rasilimali za nchi bila kujali kelele za wananchi, kuvunja kila palipojengwa, kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi na kuchukua pesa za nchi na kuzihamishia ugenini......

No comments: